Titel des Artikels: The ABC's of First Aid | Erstellungsdatum: 04/07/2014 | Aktualisiert am: 04/07/2014 | Sprache: Swahili | Kategorie: Translation | TranslatorPub.Com Rang: 215 | Views: 3838 | Kommentare: 0 | Bewertungen: 0, Bewerten Sie: 0 (10 Max)
| Text:
Swahili "Habari kuhusu huduma ya kwanza habari iliyotolewa hapa ni ya usaidizi tu ikiwa daktari hayupo."
"Usaidizi Maalum kutoka kwa daktari unafaa kutafutwa haraka iwezekanavyo!"
"Habari hii imetokana na utaalam mashuhuri uliochaguliwa kwa umakinifu."
"Tafadhali tuma ujumbe wa huduma ya kwanza kupitia Tweeter ukitumia alama za heshi inavyohitajika."
"Habari za kimsingi kuhusu huduma ya kwanza zinatumwa hapa chini. Kwanza, ______, kisha Kiswahili, hatua kwa hatua."
"Zifuatazo ni Hatua za Kwanza za Kumkagua na Kumtibu Mtu Aliyejeruhiwa."
"Kumbuka kila mara kukagua njia za pumzi, utaratibu wa kupumua na kuzunguka kwa pumzi katika mtu aliyejeruhiwa. Hatua zimeanzia hapa"
"Kila mara, tatua matatizo ya kupumua, kama vile majeraha ya kifua, kabla ya kutatua matatizo ya kuzunguka/kuvuja damu, isipokuwa ikiwa kuvuja damu kunahatarisha maisha.
"Iwapo kuvuja damu kunahatarisha maisha, kutibu kwanza na usitishe kuvuja huku!"
"Njia ya pumzi imefunguka? Baini iwapo njia ya pumzi ya mtu huyu imefungwa na chochote, kama vile kifaa cha kutoka nje ya mwili au matapishi."
"Huenda utahitaji kukigeuza kichwa na kukiinua kidevu ili kuifungua njia ya pumzi. Iwapo njia ya pumzi haijafunguka, mgonjwa huyu hawezi kupumua."
Kifua kinaonyesha mwendo? Unamsikia mgonjwa akipumua? Unahisi mapafu yakipanuka unapokagua kifua cha mgonjwa huyu?"
"Ikiwa mgonjwa hapumui, ufufuaji wa kinywa kwa kinywa unaweza kuhitajika."
"Huu ni wakati hewa inazunguka mwilini. Moyo wa mgonjwa unapiga? Je, kuna mrindimo wa damu? "Iwapo hakuna, migandamizo inaweza kuhitajika."
"Ikishabainika kwamba mgonjwa anapumua na kwamba moyo unapiga na damu kuzunguka, huduma ya kwanza inaweza kutolewa kwenye majeraha maalum."
"MWISHO wa hatua za kwanza za huduma ya kwanza, yaani hatua za kimsingi za Huduma ya Kwanza."
"Iwapo damu inavunja kwa wingi kufuatia jeraha la ajali au kidonda kilichoingia ndani sana, ni lazima kuvuja huku kudhibitiwe."
"Jambo muhimu! Ili kudhibiti damu inayovunja, utahitaji kushinikiza pande zote mbili za kidonda hasa katika vidonda vilivyo na sehemu ya kuingilia na kutokea."
"Kushinikiza hufanywa vyema zaidi mtu akivalia glavu ili kuzuia kumwambukiza mgonjwa au kujiambukiza kwa kuguza damu."
"Iwapo hakuna glavu safi, hakikisha kabisa kunawa mikono kabla na baada.
"Vifaa vinavyotumika badala vya kitambaa kilichotakaswa ni nepi safi na zilizotakaswa."
"Habari kuhusu huduma ya kwanza iliyotolewa hapa ni ya usaidizi tu ikiwa daktari hayupo." "Usaidizi Maalum kutoka kwa daktari unafaa kutafutwa haraka iwezekanavyo!"
"Habari iliyotolewa hapa imetokana na utaalam mashuhuri uliochaguliwa kwa umakinifu."
"Tafadhali tuma habari yoyote iliyo katika lugha ya Kiyukreini kwa [email protected]. Tutaitathmini na kuichapisha ili itumike. ASANTE!"
"Kumbuka kutatua matatizo ya kupumua kama vile majeraha ya kifua kabla ya kutatua matatizo ya kuzunguka/kuvuja damu, isipokuwa ikiwa kuvuja damu kunahatarisha maisha."
Tafadhali tujulishe iwapo kuna habari usiyoelewa. Tumetia juhudi zote kuhakikisha kuwa habari na hatua za huduma ya kwanza ni rahisi kueleweka. Asante!
|
|